Thursday, December 3, 2015

Anonymous

KIMENUKA MOROGORO: Afisa Ardhi Kapewa Siku 14 Za Kujieleza Kwa Nini Asifukuzwe Kazi

Katibu mkuu ofisi ya Waziri mkuu (TAMISEMI) Jumanne Sagini ametoa siku 14 kwa afisa ardhi, mhandisi wa majengo na Afisa mipango miji manispaa ya Morogoro kuandika maelezo ya kwanini wasifukuzwe kazi kutokana na kufanya kazi chini ya kiwango na kukiuka maadili ya utumishi wa umma

Agizo hilo limekuja kufuatia watendaji hao wa serikali kutumia vibaya mamlaka waliyopewa na serikali ikiwemo kuruhusu ujenzi wa hoteli ya Flomi iliyopo eneo la Msamvu, kujengwa katika eneo ambalo wanajua limepita bomba la mafuta la TAZAMA.

Pia kushindwa kuzuia ujenzi wa holela katika maeneo yasiyo rasmi pamoja na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya ofisi hizo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.