Aliyekuwa
 Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) kwa miaka mitano iliyopita, 
David Kafulila ameamriwa na Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora kulipa Sh7.5 
milioni kama dhamana, ili ombi lake lakutaka itengue matokeo ya ubunge 
wa jimbo hilo yasikilizwe.
Mahakama
 imetoa uamuzi huo kupitia kwa Jaji Leiyla Mgonya, baada ya kuzingatia 
maombi ya Kafulila aliyetaka apunguziwe gharama  ya fedha za dhamana 
kutoka Sh5 milioni badala yake alipe Sh1 milioni kwa kila mdaiwa.
Kupitia
 Wakili wake, Emmanuel Msyani, Kafulila aliwasilisha ombi Mahakama Kuu 
alipe Sh1 milioni kama dhamana kwa kila mlalamikiwa kwa kuwa hana uwezo 
wa kulipa Sh15 milioni zilizotajwa kwa mujibu wa sheria ya kesi za 
uchaguzi kwa mtu anayepinga matokeo.
Baada
 ya uamuzi huo kutolewa, alisema anakubaliana nao na yupo tayari kulipa 
kiasi hicho cha fedha ili kesi ya msingi aliyoifungua mahakamani iweze 
kusikilizwa na kutolewa hukumu.
Katika
 maombi yaliyowasilishwa na Wakili Msyani kwa niaba ya Wakili Daniel 
Lunyemela ambaye hakuwapo mahakamani, aliiomba Mahakama ikubali  ombi 
la  mteja wake kwamba, hataweza kumudu kulipa kiasi kilichokuwa 
kikitakiwa cha Sh15 milioni.
Msyani
 aliiambia Mahakama kuwa kutompunguzia gharama mteja wake ni kumnyima 
haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika chombo cha sheria kama 
ilivyoainishwa.
Upande
 wa utetezi uliowakilishwa na mawakili  waandamizi wa Serikali,  Juma 
Masanja na Kennedy Fungamtama, waliiomba Mahakama itupilie mbali maombi 
hayo kwa madai kuwa Kafulila ana mali na fedha ambazo alilipwa zaidi ya 
Sh200 milioni na kwamba, alikuwa akilipwa na Bunge kila mwezi Sh11 
milioni


Note: Only a member of this blog may post a comment.