Thursday, December 3, 2015

Anonymous

Askofu GWAJIMA Yamkuta...Wachungaji Wanne Watimka!

AMANI (1) 
Mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo waliotimka, Godfrey Benjamin.
NI SOO! Wachungaji wanne wa Kanisa la Nyumba ya Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima wametimka, Amani linaripoti.
Kwa mujibu wa mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo, Godfrey Benjamin (pichani) aliyekuwa na cheo cha Potential Shepherd (Mchungaji wa Kundi Dogo), wachungaji hao walitimka baada ya kutofautiana kuhusu matumizi ya fedha zilizochangwa na waumini miezi michache iliyopita.
gwajima2Mchungaji Josephat Gwajima.
Alidai kuwa katika moja ya ibada zake, Mchungaji Gwajima aliwaambia waumini kwamba kutokana na jua kali linalowachoma wakiwa kwenye ibada (iliyokuwa ikifanyika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Da) wanapaswa kuchanga fedha ili wanunue maturubai.

“Waumini waliitikia wito, lakini baada ya fedha kuchangwa, kiasi cha shilingi milioni 450 kilipatikana. Cha ajabu, badala ya kununua maturubai, Gwajima akawaita maaskofu na kuwaambia ni heri kununua mabasi ili kulipa hadhi kanisa. Wapo wachungaji walipinga wakitaka fedha hizo zitumike kwa makusudio ya kuchangwa kwake, lakini yeye akasisitiza kununuliwa mabasi, waliopinga wakaamua kuondoka,” alisema Benjamin.

Benjamin aliwataja wachungaji waliotimka katika kanisa hilo zaidi yake kuwa ni Winner Mbasyula, Geofrey Mwiru na William Mbasyula ambao wameanzisha kanisa lao liitwalo Kanisa la Nyumbani, Mbezi Kibanda cha Mkaa, Dar.
Gazeti hili lilifika hadi lilipo kanisa hilo na kuwakuta wachungaji hao ambapo katika mazungumzo yao kwa nyakati tofauti, walikiri kujiengua kutoka kwa mhubiri huyo maarufu kwa kile walichosema kutofautiana kuhusu matumizi ya fedha zilizochangwa na waumini.

Gazeti hili lilifanya jitihada za kila namna ili kuonana na Mchungaji Gwajima, lakini haikuwezekana ambapo katika mahubiri ya kila Jumapili ambayo yanafanyika Ubungo, walinzi wamekuwa wakiwazuia waandishi kuonana naye.
Simu yake ya mkononi nayo kila ilipopigwa haikupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi haukujibiwa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.