Ofisa Habari wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud.
Manusra hao wakiendelea na matibabu.
WATU watano waliokuwa wakichimba madini
katika mgodi wa Nyangarata uliopo Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
wamepatikana wakiwa hai baada ya kufukiwa na vifusi kwenye mashimo ya
mgodi huo kwa siku 41.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Wizara ya Nishati na Madini,
Badra Masoud amesema kuwa wachimbaji hao wanaodaiwa kuwa sita,
walifukiwa na vifusi mnamo Oktoba 5, mwaka huu na kuendelea kuishi
kwenye mashimo hayo huku wakila magome ya miti na udongo baada ya
kushiwa chakula walichokuwa nancho, hadi jana Novemba 5, walipookolewa
umbali wa kilomita 10 ndani ardhini na watano kati yao kukutwa hai huku
mwenzao mmoja akidaiwa kufariki dunia.
Baada ya kupatikana wakiwa hai, manusra
hao walikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kahama ambako wanaendelea
kupata matibabu.
Badra amewataja waliopatikana hai kuwa
ni; Joseph Bulule, Chacha Wambura, Unyiwa Aindo, Msafiri Gerald na
Muhangwa Amos. Wakati aliyefariki akimtaja kwa jina la Mussa Supana.
Tazama video hiyo hapa
PICHA NA DENIS MTIMA/GPL
Note: Only a member of this blog may post a comment.