Tuesday, November 10, 2015

Anonymous

VIDEO: Shuhudia Tukio Zima la Rais MAGUFULI Alipofanya Ziara ya Kushtukiza Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Rais John Magufuli jana alifanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa lengo la kujionea uhalisia wa huduma inayotolewa.
Kama ilivyokuwa alipofanya ziara ya kushtukiza katika Wizara ya Fedha wiki iliyopita, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa hospitali hiyo na kuongozana nao katika maeneo ambayo aliyachagua yeye.

Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini.
Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko.

Tazama video hiyo hapa

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.