Bado headlines za staa wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo zinazidi kuchukua nafasi kila siku, hii ni sehemu ya interview ya Tv Show aliyofanya Uingereza mahali ambapo alifanya uzinduzi wa movie ya maisha yake halisi inayoitwa ‘Ronaldo’ . Katika show hiyo Ronaldo alifunguka baadhi ya vitu kuhusu maisha yake binafsi.
Katika Tv show ya ‘The Jonathan Ross Show’ Ronaldo ambaye ni mchezaji bora wa Dunia mara tatu amefunguka mambo mengi kuhusu maisha yake ila hizi ni sentensi zake tatu kuhusu ligi atazocheza baada ya Real Madrid, mahusiano yake na Lionel Messi na kuhusu mama wa mtoto wake Cristiano Ronaldo Junior.
“Mimi
na Messi hatuna upinzani tunamahusiano ya kawaida, tumekuwa tukiwania
tuzo ya Ballon d’Or kwa pamoja kwa miaka nane lakini hakuna wengine
waliowahi kufanya hivyo bali ni sisi pekee, Messi amecheza klabu moja
mimi nimecheza vilabu tofauti, kiukweli tunamahusiano mazuri japokuwa
sio marafiki katika maisha ya kawaida ila kila mmoja anamuheshimu
mwenzake” >>> Ronaldo
“Kuhusu
mama wa mtoto wangu kutojulikana kwangu mimi sioni tatizo wapo watoto
wengi duniani hawana mama, Cristiano Junior anaye baba mzuri,bibi na
suport kutoka katika familia yangu, naona ni sawa tu, najua watu
wanajiuliza kwa nini hayupo wazi kiukweli kuna vitu katika maisha ni
private na watu wanapaswa kuheshimu lakini Cristiano Junior atakapokuwa
nitamwambia ukweli kuhusu mama yake ila siwezi kusema sababu watu
wanataka niseme” >>> Ronaldo
“Katika
akili yangu nimepanga kustaafu soka katika vilabu vya juu na vyenye
ushindani na heshima kwangu lakini haina maana ya mimi kwenda kucheza
Qatar, USA au Dubai sio vizuri kwangu lakini siwezi kujua ya mbele” >>> Ronaldo
Hapa nimekuweka video hizo mbili za mahojiano hayo, bonyeza play kucheki au download kupakua
Hapa nimekuweka video hizo mbili za mahojiano hayo, bonyeza play kucheki au download kupakua
Note: Only a member of this blog may post a comment.