Thursday, November 26, 2015

Anonymous

Sentensi 7 za MBOWE Baada ya Kushinda Kesi ya Marehemu MAWAZO Jijini Mwanza (+Audio)


Ishu ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kuzuiwa kuaga mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Geita imekuwa ikiripotiwa na kuandikwa kwenye vyombo vya habari huku ikisubiriwa kutolewa majibu na Mahakama Kuu Mwanza kuhusu hatma ya zuio hilo.

Leo maamuzi ya Mahakama Kuu Mwanza yametoka na majibu kwamba wanaCHADEMA na viongozi wao wamepata kibali cha Mahakama hiyo kuendelea na shughuli za kuaga pamoja na mazishi ya kiongozi huyo.

Marehemu Alphonce Mawazo kwenye Jukwaa la Kampeni enzi za uhai wake.
Nje ya Mahakama Kuu Mwanza, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe alipata dakika chache kuongea na wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wakisubiri kusikia maamuzi ya Mahakama >>>> “Ni lazima tukae vikao kupanga ratiba ya kumuaga Kamanda Mawazo, Jaji ametoa maelekezo kwamba viongozi wa CHADEMA, familia ya marehemu na Jeshi la Polisi wakae pamoja kupanga ratiba kamili.”

“Tutaheshimu maelekezo ya Jaji lakini hatutakubali kuonewa, muwe na imani kwamba haki itatendeka… tunakwenda kwenye vikao lakini tunahitaji kumaliza jambo hili kuanzia kesho, tutamuaga Mawazo kwa heshima anayostahili katika eneo ambalo tutawatangazia.” >>> Freeman Mbowe.

Ezekiel Wenje na Salum Mwalimu wakiwa ndani ya Mahakama Mwanza.


Watu wa usalama nje ya Mahakama Kuu Mwanza.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wanaCHADEMA


Wakili wa CHADEMA, John Mallya.

Hii hapa sauti ya Freeman Mbowe nje ya Mahamaka Kuu Mwanza.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.