Thursday, November 19, 2015

Anonymous

Prof. JAY Ndani ya Mjengo Bungeni? Dully + Yamoto Band? Msami Feat. Tekno? #255

Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule a.k.a Professor Jay tayari ameingia ndani ya Bunge Dodoma Tanzania… Proj. Jay amesema amefurahi kwa kuaminiwa na wananchi wa Mikumi Morogoro kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge, amefurahi na anaamini kuanzia sasa ataendelea kushughulikia majukumu yake kama Mbunge.

Joseph Haule+Joseph Mbilinyi ndani ya Bunge… YES, ni majina makubwa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyochimbukia muziki wa Rap Bongo… wao wamesema ni wawakilishi wa wale waliowachagua na kazi yao ni kuhakikisha wanatumikia wananchi kwa kutekeleza ahadi.

Wabunge Mchungaji Peter Msigwa, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Joseph Haule ‘Prof. Jay’.
Shavu jingine limewakuta Yamoto Band kufanya collabo na mkongwe Dully Sykes… Dully amesema tayari video ya mdundo wao imekamilika na kwa sasa wanatarajia kuachia video siku ya Ijumaa wiki hii.

Dully Sykes.
Kama hujui mama yake Dully Sykes ni shabiki wa muziki wa Hip Hop, Dully amesema kwa sasa mama yake anasikiliza sana wimbo wa Joh Makini Feat. AKA– Don’t Bother.

Msami Feat. Tekno? Good news ikufikie kwamba Msami Baby mkali wa kuimba na kudance ambaye aliibukia THT tayari ana collabo na Tekno kutoka Nigeria ambaye amekamata headlines sasahivi na mdundo wa ‘Duro‘.

Msami Baby.
Msami amesema mipango inayofatia sasahivi ni kujiandaa kuachia ngoma hiyo watu waisikie pamoja na video kama mambo yakienda sawa.

Msanii Tekno kutoka Nigeria.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.