PAPA Francis wa Kwanza ameongoza ibada
ya misa ya kwanza leo barani Afrika akiwa nchini Kenya ambayo
imehudhuriwa na maelfu ya watu katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi
akisisitiza umuhimu wa kuheshimu familia katika jamii.
Awali katika mkutano na viongozi wa dini mbalimbali, alisema dini haifai kutumiwa kuvuruga amani kwani “Mungu ni Mungu wa amani.
“Jina lake takatifu halifai kutumiwa
kutetea chuki na mauaji. Ninajua kwamba mashambulio ya Westgate, Chuo
Kikuu cha Garissa na Mandera bado hayajasahaulika. Na sana, vijana
wamekuwa wakiingizwa na kufunzwa itikadi kali kwa jina la dini,
kupandikiza woga na kuvunja umoja katika jamii,” alisema.
“Ni muhimu sana tuwe manabii wa amani,
watu wa amani wanaokaribisha wengine kuishi na amani, umoja na
kuheshimiana. Mungu na akaguse mioyo ya wanaohusika katika mauaji na
ghasia, na azipe imani familia na jamii zetu.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.