Yusuf Ramadhan.
Haruni Sanchawa
KIFO njenje! Kijana Yusuf
Ramadhan (26), mkazi wa Chamazi jijini Dar, amenusurika kuuawa baada ya
kupigwa risasi shavuni na mtu anayesadikika kuwa ni jambazi aliyekuwa
amelenga kumpora pikipiki yake aina ya boksa.
Akisimulia mkasa huo akiwa amelazwa
kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar, kijana huyo alisema
kwamba, ilikuwa hivi karibuni ambapo alikodiwa na abiria kutoka maeneo
ya Mbande hadi Chamazi.
Alisema kuwa alipofika sehemu huko
Chamazi, abiria huyo alimwambia amefika hivyo amshushe, akiwa bado
anasubiria kulipwa ndipo akatokea mtu porini na kumpiga risasi ya shavu
la kulia.
Kijana Ramadhani anaishi na risasi hiyo
kwenye shavu la kulia akiwa amelazwa kwenye wodi namba 23 katika Jengo
la Sewa Haji Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.
Majeruhi huyo anaomba msaada kwani hali yake kiuchumi baada ya kupatwa na masaibu hayo imekuwa mbaya na ndugu zake hawana uwezo.
“Hapa nilipo nipo katika wakati mgumu
kifedha na kuna mahitaji mengi yanahitajika hivyo nawaomba Watanzania
wenzangu wanisaidie ili niweze kujikimu,” alisema kijana huyo.
Kwa yeyote aliyeguswa na habari hii anaweza kuwasiliana naye kwa kutumia simu 0717 099635.
Note: Only a member of this blog may post a comment.