
Jana Balozi Sefue alisema baada ya Bendera ya Rais kuteremshwa na kabla Bendera ya Rais mpya kupandishwa, magari ya mawaziri na Naibu Mawaziri, yatabadilishwa namba kwa kuondoa herufi ya cheo chake (W au NW) na kurejeshwa kwenye namba za serikali (ST).
Balozi Sefue alisema baada ya shughuli hiyo, magari hayo yatawarudisha nyumbani mawaziri na naibu Mawaziri waliomaliza muda wao na kurejeshwa Ikulu tayari kwa ajili ya kupewa mawaziri wapya watakaoteuliwa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.