Good Morning mtu wangu, ni jumatatu
nyingine na kama kawaida lazima tuanze na Uchambuzi wa Magazeti
@CloudsFM. Inawezekana baadhi ya stori kubwa kwenye kuperuz na kudadis
zimekupita, nimezisogeza zile zote za leo hapa chini.
Saa 72 zabaki za Magufuli kuwashughulikia mafisadi na majizi, Mawaziri waweweseka, nusu yao hawana nafasi Baraza la Mawaziri la Dk. John Magufuli… Ibrahim Lipumba ashitushwa na kauli iliyotolewa na mwenyekiti wa ZEC Zanzibar akidai mwenyekiti huyo hakufanya haki kwa kutowashirikisha macommissioner wengine.. Bidhaa Zanzibar zapanda
bei baada ya meli zinazosafirisha bidhaa hizo kupunguza safari za
kwenda visiwani huko kutokana na hali ya kisiasa iliyopo visiwani humo.
Wakati sintofahamu juu ya hali ya Zanzibar ikiendelea, Rais Jakaya Kikwete ameiamuru ofisi yake kusaidia kufanikisha mazungumzo kati ya mgombea Urais wa CUF Maalim Seif na Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama General Davis Mwamunyange… Kilichoharibu kura zaidi ya laki nne yawekwa hadharani, huku NEC ikisema sababu kuu ikiwa ni elimu ya uraia na ya mpiga kura kutokuwafikia wananchi kwa usahihi.
Uchaguzi wa Ubunge kwa majimbo ya Handeni na Arusha mjini umepangwa kufanyika tarehe 12 December 2015 ambapo Mkurugenzi wa NEC jana amesema hivi karibuni watatangaza kuanza kwa kampeni baada ya kupitisha majina ya wagombea, Majimbo ya Lushoto na Ulanga Mashariki uchaguzi kufanyika tarehe 22 November lakini kampeni sehemu hizo zimeshaanza huku majimbo ya Ludewa na Masasi mjini taratibu zake kutangazwa hapo badaae.
Aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Kigomba Kusini kwa ticketi ya Chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila ametengaza kukata rufaa kupinga matokeo ya Uchaguzi uliompatia ushindi mgombea wa Chama cha CCM kwenye nafasi hiyo, uamuzi huo ameubainisha jana jijini Dar es salaam baada ya kuzungumza na waandishi wa habari.
Tunaomba radhi kutokana na tatizo la sauti.

Note: Only a member of this blog may post a comment.