WATU
wengi wenye uzito wa kupindukia au ule unaowakera wamekuwa wakipambana
kwa nguvu zote ili kupungua bila kuelewa kuwa, kuufanya mwili uwe mnene
au uzito mkubwa ni rahisi kuliko kuupunguza.
Ni kama kujenga nyumba. Nyumba inaweza kujengwa kwa mwaka mmoja lakini kuibomoa isizidi saa sita. Leo tunawaletea ratiba ya vyakula ambavyo, mtu mnene na anayetaka kupungua, akila atafanikiwa kupungua uzito au unene.
Siku ya kwanza asubuhi matunda. Lakini hayo matunda usitumie kabisa ndizi. Mchana chemsha kabichi yako, iweke chumvi kidogo na nyanya ili upate supu halafu kunywa mchanganyiko huo.
Jioni yake kula tunda la tikitimaji na mbogamboga za majani au kabichi. Unaweza kutumia kabichi uliyoiandaa mchana kama ilibaki na ukaitunza vizuri.
Siku ya pili kula mboga za majani asubuhi lakini usile mboga za majani zenye wanga mwingi kama wa kwenye karoti. Mchana wake kula kabichi iliyochemshwa na kuungwa pilipili na mafuta kiasi ukiwa umetengeneza na kachumbari.
Jioni pata mlo kama wa mchana lakini unaweza kukaanga mboga nyingine za majani kama zipo, si mbaya sana.
Siku ya tatu unaweza kula mboga za majani, wmatunda na kiazi kitamu kimoja mpaka viwili.

Siku ya nne mlo wako uwe ndizi moja na unywe na maziwa ya mtindi wakati wa asubuhi. Mchana kula kabichi kama ulivyoitengeneza kwenye siku ya kwanza. Usiku rudia mlo wa mchana.
Siku ya tano unaweza kupata nyanya mbichi ukiwa umechanganya na samaki au kipande cha kuku aliyekaangwa. Hiyo ni asubuhi.
Mchana wake shiriki mlo wa samaki aliyechemshwa kiasi na pia akachanganywa na nyanya. Jioni yake hakikisha unafukia tumboni chakula kama cha mchana.
Siku ya sita kula chakula cha protini chenye mchanganyiko na mboga za majani. Anza siku kwa kula kachumbari asubuhi. Mchana kula tambi kiasi na kipande kidogo cha samaki. Usiku tengeneza supu ya kabichi.

Siku ya saba asubuhi kula matunda kisha kunywa juisi. Mchana kula mboga za majani na usiku kula supu ya kabichi na kiazi kimoja.
Ushauri; ni vizuri kabla ya kuanza kupata mlo wenye ratiba hii ukapima uzito wako ili siku ya saba upime tena kujihakikishia zoezi kwenda vizuri.
Note: Only a member of this blog may post a comment.