Tuesday, November 10, 2015

Anonymous

Kisa UCHAGUZI Steve NYERERE na JB Wamelishwa Sumu? Ramani ya Luteni Kalama South Africa? Majibu Haya Hapa..


Gangwe Mobb ni kundi ambalo kama ukiitaja safari ya Bongo Fleva Tanzania, huwezi kuacha kulitaja kundi hilo lililoundwa na Luteni Kalama pamoja na Inspector Haroun.

Luteni Kalama na Inspector Haroun
Luteni Kalama amesimulia kwamba kuna time alikuwa na mipango ya kuzamia South Africa, rafiki yake mmoja alimchorea ramani ya safari nzima mpaka atakapofika.

Baada ya kukutana na Inspector Haroun alimshirikisha kuhusu mipango yake hiyo huku wakiendelea kufanya shughuli za muziki… Kalama anasema baadae ramani yake ilipotea kwa hiyo hata mpango wa safari haukuwepo, lakini baada ya muda alikuja kujua kwamba kumbe ramani yake haikupotea ila Inspector Haroun aliificha !! Mipango ya safari ikaishia hapo wakaendelea na muziki.

Mwigizaji JB
Kuna stori kuhusu Steve Nyerere na JB kulishwa sumu, na ishu inahusishwa na Uchaguzi, kuna ukweli ??
JB amesimulia ilivyokuwa kwamba walikuwa pamoja wakala chakula kwenye sehemu tofauti… baadae JB amesema aliumwa sana tumbo akaamua kwenda Hospitali, baada ya kufanyiwa vipimo alipatiwa matibabu.

Mwigizaji Steve Nyerere
Kuhusu ishu ya sumu, JB amesema haamini kama chakula hicho kilikuwa na sumu ila alichoambiwa Hospitali ni kwamba chakula kilikuwa kibovu na tayari amepatiwa matibabu japo maumivu ya tumbo aliyoyapata yalikuwa makali sana.

Q Chief
Q Chief na Harmonize ndani ya studio, walishirikiana kufanikisha mdundo wa Q Chief? Harmonize alisimulia kwamba alishiriki kuandika verse moja ya wimbo wa ‘Mdogo Mdogo‘ wa Q Chief, leo 255 iko na Chillah mwenyewe ambaye amesema ni kweli kuna mawazo ya Harmonize yaliyosaidia kukamilisha verse ya pili kwa sababu wakati ngoma hiyo inafanywa walikuwa pamoja studio.

Harmonize

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.