Gladness Mallya
Aliyekuwa mke wa Emmanuel Mbasha, Flora Mbasha
Emmanuel Mbasha na mkewe
MWIMBAJI wa nyimbo za Injili na
mfanyabiashara maarufu Bongo, Emmanuel Mbasha amepotezea kuzungumzia
suala la kumpa talaka mkewe kwa madai kwamba yupo bize na suala la
sherehe za ushindi wa rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli.
Mbasha aliitoa kauli hiyo hivi karibuni
wakati mwanahabari wetu alipomuuliza mwimbaji huyo kuhusu hatma ya kutoa
talaka ambayo aliyekuwa mkewe, mwimbaji Flora Mbasha amekuwa akiidai
hadi kumfikisha mahakamani.
“Sikia bwana, mimi kwa sasa nipo bize na
sherehe za ushindi wa Magufuli siwezi kupoteza muda wangu kuzungumzia
vitu vidogovidogo kama hivyo, kwangu mimi rais wa nchi ni muhimu kuliko
hayo mambo ya Flora unayoniulizia,” alisema Mbasha.
Emmanuel na Flora walikuwa wanandoa na
kubarikiwa kupata mtoto mmoja kisha kugombana na kufikia hatua ya
kuachana na sasa kila mmoja anaishi kivyake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.