Kimenuka Jimbo la Kinondoni...Aliyekuwa Mgombea wa Ubunge KALAPINA Kupinga Matokeo Mahakamani...Adai Mawakala Wake Walifanyiwa Kitu Mbaya
ALIYEKUWA mgombea Mbunge katika Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama
cha ACT-Wazalendo, Kalama Masoud ‘Kalapina’ ameibuka na kupinga matokeo
akidai atakwenda mahakamani.
Akizungumza na wanahabari leo Makao Makuu ya chama hicho Kijitonyama
jijini Dar es Salaam, Kalapina amesema matokeo yaliyompa ushindi mgombea
wa chama cha wananchi CUF ambaye alikuwa anaungwa mkono na vyama
vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Abdul Mtulia yalikuwa
yamesheheni dosari kubwa.

Amesema katika kata 19 zilizopo katika Jimbo la Kinondoni, mawakala wake
walitishiwa na kulazimika kuacha kusimamia vituo walivyokuwa
wamepangiwa.Kalapina alitaja baadhi ya maeneo aliyodai mawakala wake
walitishiwa na baadae kuamua kuondoka kuwa ni kata za
kijitonyama,Tandale, Ndugumbi pamoja na Kigogo.
Alieleza kuwa baada ya kubaini matatizo yote hayo alilazimika kugomea
kusaini karatasi ya wagombea ubunge, akiongeza kuwa hatua iliyobaki kwa
sasa ni kwenda kufungua kesi mahakamani.“Natarajia kwenda mahakamani
kutaka haki, kwa hiyo Jumatatu au Jumanne ijayo nakwenda kufungua kesi,”
alisema kalapina.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.