LICHA ya Ligi Kuu Bara kusimama,
mpaka sasa katika orodha ya wafungaji wa ligi hiyo, Shomari Kapombe ni
beki pekee ambaye amefunga mabao mengi na kuweza kuwafunika baadhi ya
mastraika katika ligi hiyo huku wengi wakiwa hawana bao hata moja.
Kapombe amefanikiwa kufunga mabao manne
na kuwafunika mastraika kama Mussa Hassan ‘Mgosi’, Pape N’daw (wote
Simba) ambao hawana bao hadi sasa, wengine ni kama Themi Felix (Mbeya
City), Abasirim Chidiebere (Coastal Union) na wengineo.
Msimu wa mwaka 2013/14, Tumba Sued akiwa
na Ashanti United alifanikiwa kuwa beki aliyefunga mabao matano akiwa
beki pekee ambaye alifunga mabao mengi na kuweza kuwafunika baadhi ya
washambuliaji mpaka ligi ilipokuwa inamalizika
Mpaka sasa imechezwa michezo kumi huku
wengine wakiwa wamecheza michezo tisa na tayari mabao jumla yaliyofungwa
ni 144, ligi imesimama huku kinara wa mabao akiwa mshambuliaji wa Stand
United , Elias Maguli mwenye mabao tisa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.