Najua tumeshawahi kukutana na stori
kuhusu hukumu za kifungo cha miaka kadhaa mpaka 30 jela, au wengine
wanahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kufanya makosa mbalimbali…
lakini kuna hukumu ambazo ukitajiwa namba za miaka yake unaona bora kama
hukumu yenyewe ingekuwa tu kifungo cha maisha !! Miaka 885 jela,
anatoka mtu kweli hapo ?!
Shawn Ryan Thomas
alidakwa na Polisi Florida Marekani akiwa na picha za utupu za watoto
wadogo, kesi ikafika Mahakamani na hukumu yake ikatolewa kwamba
atatakiwa kutumikia jumla ya miaka 885 jela.
Ripoti nyingine kutoka Florida Department of Law Enforcement imesema Thomas alinaswa pia akiwa kwenye mpango wa kumteka msichana mwingine mdogo, kuwaua wazazi wake na kumrekodi mkanda wa utupu !!
Stori yake iko kwenye Video pia mpaka Mahakama ilivyomsomea hukumu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.