Wednesday, November 11, 2015

Anonymous

Je, Kununua Magari Zaidi ya 700 Kwa Ajili ya Polisi Wakati Wagonjwa Wanalala Chini Mahospitalini na Vifaa Havifanyi Kazi ina Tija Kwa Taifa?

Nilisikitika sana kuona Rais mstaafu JK akiagiza Magari zaidi ya 700 kwa ajili ya Polisi.
Kinachonisikitisha na kunishangaza ni kwamba je tulikuwa na haja ya kuagiza magari mengi namna hiyo? 

Turudi kwenye uhalisia wa mambo ya msingi.
Ukienda kwenye Hospitali za Serikali, Hakuna madawa, Mashine za CT scan zimeharibika wakati huo huo wagonjwa wakilala chini kwa kukosa vitanda.
Wanafunzi wa vyuo vikuu wanakosa mikopo na kukosa haki za kupata elimu.
Sasa nauliza je kulikuwa na umuhimu gani wa kuagiza magari kama hayo wakati kuna mambo mengi yanaharibika kwa fedha kukosekana?

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.