Mbunge mteule wa Butiama Nimrodi Mkono wa CCM ndiye mwenye umri mkubwa zaidi kuliko wabunge wote waliotangawa na tume ya Taifa ya uchaguzi NEC.
Mkono anashikilia rekodi hiyo ya kuwa mbunge mwenye unri mkubwa
kuliko wenzake wote akiwa na umri wa miaka 72 akifariwa na Mbunge wa
Urambo Mashariki Margaret Sitta mwenye umri wa miaka 69.
Kwa mujibu wa orodha ya wabunge wa bunge la 11 iliyotolewa jana
Mkurugenzi wa NEC Ramadhan Kailima, mbunge menye umri mdogo ni wa jimbo
la Kasulu vijijini Holle Vuma kupitia CCM mwenye miaka 25.
Katika Bunge lililopita aliyekuwa Mbunge wa Muhambwe kupitia NCCR, Felix Mkosamali ndiye aliyekuwa na umri mdogo wa miaka 24.


Note: Only a member of this blog may post a comment.