Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars bado haina hali nzuri sana ya kujihakikishia inashinda mchezo wake wa marudiaono dhidi ya Algeria baada ya mchezo wa kwanza uliyochezwa November 14 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam na kumalizika kwa sare ya goli 2-2., matokeo ambayo hayatajwi kuwa mazuri sana kwa Taifa Stars ukilinganisha wanaenda kucheza ugenini.
Taifa Stars ambayo imesafiri leo November 15 kuelekea Algeria na imewasili salama imeahaidiwa milioni 500 na kamati ya ushindi ya Taifa Stars, kamati hiyo imetangaza dau hilo kama motisha iliwaweze kucheza na kupata matokeo mazuri, mchezo wa kwanza Taifa Stars waliahidiwa milioni 50 kama wangeshinda ila wamepewa milioni 25 baada ya kutoa sare.
Kiwango kilichotangazwa na kamati ya ushindi ya Taifa Stars
ni mara kumi ya dau walilokuwa wameahidiwa awali, hivyo hii ni jinsi
ambavyo kamati ya ushindi imeipa uzito mechi hii, majirani wa Tanzania timu ya taifa ya Uganda imefanikiwa kuwa timu ya kwanza ya Afrika Mashariki kufuzu hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi. Taifa Stars itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya Algeria Jumanne ya November 17 Algeria.
Note: Only a member of this blog may post a comment.