Gladness Mallya
SIRI nzito!
Imebainika kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe
Magufuli ana siri nzito na siku ya Alhamisi kwani matukio yote muhimu
na makubwa yameonesha kujitokeza kwake ndani ya siku hiyo.
Akizungumza na gazeti hili juzi,
mtaalamu wa mambo ya nyota nchini, Maalim Hassan Yahya alisema Dk.
Magufuli ana siri nzito na siku ya Alhamisi ambayo inaonesha mambo
mazuri kwake na nchi kwa ujumla.
Alieleza kwamba, siri hiyo inaanzia
mwaka huu ambao unatawaliwa na nyota ya Mshale na Samaki, ulianza siku
ya Alhamisi (Januari Mosi), kutangazwa kwake Dk. Magufuli kuwa rais pia
ilikuwa siku ya Alhamisi (Oktoba 29) ambayo pia ilikuwa ni siku yake ya
kuzaliwa.
Mbali na Alhamisi hizo, lakini pia
utafiti unaonesha hata mwaka huu utaisha siku ya Alhamisi hivyo
kuongezea usiri mkubwa wa siku hiyo kwa Rais Magufuli.
Kama hiyo haitoshi rais huyo aliapishwa
siku ya Alhamisi (jana) ambapo inaonesha katika uongozi wake utakuwa wa
mafanikio, wananchi maisha yao yatabadilika kwani kiongozi huyo
ameonekana kuwa ana nyota kali.
“Uongozi wa Dk. Magufuli utakuwa mzuri
sana maana nyota zimeonesha na hata malaika wanaotawala siku ya Alhamisi
ambayo imeonesha kuwa na matukio mengi kwake ni wazuri hivyo Watanzania
watarajie Tanzania mpya yenye neema,” alisema Maalim Hassan.

Note: Only a member of this blog may post a comment.