Mayasa Mariwata
MASTAA wa
filamu Bongo Alice Bagenzi ‘Rayuu’ pamoja na Skyner Ally ‘Skaina’
wanadaiwa kufanya uchafu baada ya picha za wawili hao wakionesha mahaba
hadharani kusambaa.
Chanzo kinaanika kuwa wawili hao hivi
karibuni walikutana katika Ukumbi wa KD, Kijitonyama ambapo kulikuwa na
sherehe ya kuzaliwa kwa Rayuu huku wakionesha mahaba ya mtu na mpenzi
wake ndipo picha hizo zilipopatikana.
“Sina tabia chafu, yale yalikuwa ni
mambo ya Kizungu tu maana ilikuwa bethidei na mwenyewe (Skaina) katika
kipindi cha kulishana keki aliamua kutumia mdomo,” alisema Rayuu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.