Friday, October 23, 2015

Anonymous

Ufafanuzi wa TAARIFA ya Uongo na Upotoshaji Kuhusu Jaji Mkuu Kukubali Wananchi Kukaa Mita 200 Iliyotolewana EATV

 
2.0 Taarifa hii si ya ukweli na ni ya upotoshaji,Mhe Jaji Mkuu hajawahi kuzungumzia chochote kuhusu sheria hiyo ukitilia maanani kesi hiyo iko Mahakama Kuu shauri Namba 37 ya 2015 iliyofunguliwa na Bi. Amy Kibatala dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Uchaguzi (DE) na itatolewa maamuzi kati ya tarehe 22 au 23 mwezi huu. Hivyo, kwa mujibu wa sheria Mhe.Jaji Mkuu asingeweza kuzungumzia chochote kuhusu sheria hiyo kwa kuwa suala hilo liko MAHAKAMANI.
3.0 Tulimwandikia Mkurugenzi wa Habari MAELEZO nakala East Africa Television na kufuatilia kwenye Baraza la Habari (Media Council) kuomba maelezo ya kina na usahihi wa taarifa hiyo, tarehe 21/10/2015 tumepokea barua Kumb Na EATV/ADMN/096/10/2015 ilyosaniwa na Bi Regina Mengi Mkurugenzi Mtendaji wa East Africa Television akiomba msamaha kuhusu taarifa hiyo potofu na kuwa watatoa maelezo ya ziada kuwa, taarifa hiyo haikutolewa na Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania.

Tunashukuru kwa ushirikiano mkubwa tulioupata toka uongozi wa juu kabisa wa East Africa Television kwa kuomba radhi mapema na Tunamini kuwa, vyombo vya Habari na Wananchi kwa ujumla vitasitisha usambazaji wa taarifa hii iliyokuwa si sahihi.
Barua ya kuomba radhi imeambatanishwa:

Imetolewa na:
MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA
MAHAKAMA YA TANZANIA

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.