Stori: Musa Mateja
KITUMBO cha mwigizaji Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kimezua
minong’ono ya aina yake kutoka kwa mashabiki na mastaa mbalimbali na
kuwafanya wengi wao wabaki wakibishana kuwa mrembo huyo atakuwa
katundikwa ujauzito na mchumba wake Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
“Huyu atakuwa kanasa si bure,” alisikika mmbeya mmoja ambaye hakujitambulisha.
Alipoulizwa Shilole kama ni kweli amenasa ‘kibendi’, alijibu:
“Jamani sina mimba, watu watambue tu kwamba hiyo picha nilikuwa nimetoka kula, lakini pia wajue kwamba siku nikipata mimba watajua tu maana nitapiga picha za kutosha,” alisema Shilole.

Note: Only a member of this blog may post a comment.