BAADA ya kubamba na Ngoma ya Kibakubaku, Khaleed Mohamed ‘TID’ amesema kuwa kwa sasa yuko ‘chimbo’ akijiandaa kuja na vitu adimu ambavyo anaamini atarejesha heshima katika soko la muziki wa Bongo Fleva.
“Niko chimbo kwa sasa, nilitulia kidogo ili niusome mchezo mzima wa gemu, nataka kurejesha heshima yangu ya enzi za Nyota Yako na Asha, mimi ni mfalme katika muziki, niko vizuri na ni kipaji changu halisi, sibahatishi,” alisema TID.

Note: Only a member of this blog may post a comment.