MKONGWE kwenye sanaa ya filamu Bongo,
Jacob Stephen ‘JB’ amefunguka kuwa rais wa awamu ya nne anayemaliza muda
wake, Jakaya Kikwete anaondoka madarakani akiwa ametoa msaada mkubwa
sana katika sanaa.
Akizungumza na mwanahabari wetu hivi
karibuni, JB alisema Rais Kikwete alikuwa akitoa msaada mkubwa sana kwa
wasanii ikiwemo kushiriki katika masuala yao ambayo uwepo wake tu
ulitosha kuifanya sanaa izidi kujulikana na kupiga hatua.
“Kikwete ametoa ushauri wa mawazo.
Amekuwa akishirikiana nasi katika shida na raha. Kutuzungumza tu katika
hadhara kwetu sisi ni jambo kubwa, tutamkumbuka kwa mengi sana,” alisema
JB.
Note: Only a member of this blog may post a comment.