Thursday, October 22, 2015

Anonymous

PICHAZ+MAELEZO: Shuhudia Alichokifanya DK MAGUFULI Jijini Dar Jana!

magufuli (1)Dk John Pombe Magufuli wakati makitoka Mwanza, alikutana na na rais Jakaya Kikwete kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwl Julius Nyerere, Dar aliyekuwa akielekea Luvuma kuwaaga wananchi wa Mkoa huo.mbagalaDk Magufuli akilakiwa na wakazi wa Mbagala-Zakhiem.magufuli (2) magufuli (3) magufuli (4) Magufuli akiwahutubia wakazi wa Mbagala, Dar mapema leo.magufuli (5)Magufuli akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Mbagala Kuu kwa tiketi ya CCM, Yusuph Manji.
TANDIKA MWEMBE YANGA (2)-001Miss Tanzania namba moja mwaka 2014, Sitti Mtemvu aliyevua taji hilo siku chache baada ya kuchaguliwa, hapa akisalimiana na Dk Magufuli katika Viwanja vya Tandika Membeyanga, Dar.BIAFRAMagufuli akimwaga sera katika Viwanja vya Biafra.UWANJA WA TP SINZA
Magufuli akimwaga sera katika Viwanja vya TP TP Sinza.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli leo ametoka jijini Mwanza kuingia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kampeni za lala salama kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika jumapili hii. 

Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl julius Nyerere, Magufuli alikutana na kusalimiana na rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Ruvuma kuwaaga wananchi wa mkoa huo. 
Baada ya hapo Magufuli aliendelea na ratiba yake ya mikutano ya kuomba ridhaa kwa wakazi wa Dar es Salaam. Maeneo amabyo magufuli amefanya mkampeni leo ni pamoja na Kigamboni katika Uwanja wa Machava, Mbagala Zakhiem, Ubungo Bus Terminal, Ubungo Shekilango, Tandika Mwembeyanga,  Uwanja wa TP Sinza na kumalizia mkutano mkubwa katika viwanja vya Biafra. 

Akiwahutubia wananchi wa Kigamboni, Magufuli aliwatoa hofu kuwa hakuna atakayedhurumiwa kufuatia ujenzi wa mjiwa kisasa katika eneo hilo. pia alisema eneo hilo atalifanya kuwa wilaya mpya ili liwe na hadhi na kupewa huduma zote kama jimbo linalojitawala. Baada ya kuwa wilaya ataipatia Hospitali ya Wilaya na huduma zingine zitaongezwa. 

Akiwa maeneo mengine, Magufuli aliwanadi wabunge na madiwani wanaowania nafasi hizo kwa tiketi ya CCMhuku akiwaahidi wananchi kuwaboreshea maisha, kupambana na rushwa na mafisadi.
Pia aliongeza kuwa, daraja la Kigamboni linatarajiwa kukamilika mwezi ujao ambapo wananchi watavuka bure.
PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.