Aliyekuwa katibu wa vijana Wilaya ya Hai Jubiliat Lema kushoto baada ya kurudisha kadi.
Nchimbi akiwashauri Wanasiha kumchagua Magufuli na kuzieleza sifa zake.
Mgombea ubuge jimbo la Moshi Mjini, Davis Mosha mwenye shati la njano akipiga push up sambamba na wagombea Udiwani.
Mgombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini Davis Mosha akicheza Rege na Madee na Tundaman.
Nature na Rich One wakikamua.
Nature akikumbatiana na Magufuli.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Yanga, Jerry Muro na Maimarth Jesse nao walikuwepo kwenye mkutano wa
Magufuli uliofanyika Moshi mjini.
Magufuli akisalimiana na wakazi wa Arumeru Mashariki.
Wakazi wa Arumeru wakimsapoti Magufuli kwa kupiga pushap.
Mapaparazi wakiwa kazini kama walivyonaswa kwenye mkutano wa Magufuli uliofanyika Sanya Juu Wilaya mpya ya Siha.
Wakazi wa Sanya juu Jimbo la Siha wakimsubiri Magufuli awamwagie sera.
Wakazi wa Sanya juu wakimshangilia Magufuli (hayupo picha).
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi jana
alifanya mikutano zaidi ya saba kwenye viunga mbalimbali vya mkoa wa
Kilimanjaro. Miongoni mwa maeneo aliyonadi sera zake za matumaini ni
Ngarasero, Njia Panda ya Kia, Sanya Juu Wilayani Hai, Bomang’ombe,Rau,
Uru Shimbo Jimbo la Moshi Vijijini na kumalizia kwa mkutano mkubwa
uliofurika umati watu.
Katika mikutano hiyo Magufuli aliwaahidi wakazi hao kuwamalizia
tatizo la maji, kusambaza umeme sehemu ambazo umeme haujafika, na kuwapa
kilometa 10 za barabara. Licha ya ahadi hizo Magufuli aliwaahidi wakazi
hao kuwatatulia migogoro ya ardhi sehemu mbalimbali za mkoa huo.
Katika mkutano huo viongozi kadhaa wa Chadema walirudisha kadi kwa
Magufuli na kumuahidi kumuunga mkono katuka harakati zake za kuwania
urais.
(Habari/Picha: Richard Bukos)

Note: Only a member of this blog may post a comment.