GLADNESS MALLYA
MREMBO anayedai kuzaa na mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’, Ester Eliakim amekwenda polisi, Kituo cha Stakishari kumshtaki mwigizaji huyo akidai hampi matumizi ya mtoto anayedai kuzaa naye.
Licha ya Dude kumkana motto huyo, mrembo huyo amesema ana uhakika
mtoto huyo amezaa na Dude lakini kinachomsikitisha kila anampomuomba
matumizi, staa huyo amekuwa akimtukana badala ya kumjibu vizuri.
“Nimempeleka polisi pale Stakishari. Nikapelekwa Dawati la Jinsia.
Amepigiwa simu ya kuitwa akadai hayupo Dar na kuahidi akirudi atafika
ili tutafute muafaka,” alisema Ester.
Alipotafutwa Dude kuhusiana na ishu hiyo, aliendelea kusisitiza kwamba hamtambui mrembo huyo bali anataka kujitafutia umaarufu kupitia jina lake.
“Nilishasema simjui huyo mtu bwana, aniache, atakuwa anatafuta umaarufu tu,” alisema Dude.
MREMBO anayedai kuzaa na mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’, Ester Eliakim amekwenda polisi, Kituo cha Stakishari kumshtaki mwigizaji huyo akidai hampi matumizi ya mtoto anayedai kuzaa naye.
Alipotafutwa Dude kuhusiana na ishu hiyo, aliendelea kusisitiza kwamba hamtambui mrembo huyo bali anataka kujitafutia umaarufu kupitia jina lake.
“Nilishasema simjui huyo mtu bwana, aniache, atakuwa anatafuta umaarufu tu,” alisema Dude.
Note: Only a member of this blog may post a comment.