Thursday, October 22, 2015

Anonymous

MAPYA Yaliyojiri Kesi ya Mita 200 Leo Mahakama Kuu Jijini Dar

3.Dk. akifanya mahojiano na wanahabri.
Wakili wa serikali Dk.Tulia Ackson akifanya mahojiano na wanahabari
4.Wakili Peter Kibatala wa upande wa mlalamikaji akitoka katika chumba cha mahakama kwenye kesi hiyo
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania leo imehairisha tena kesi namba 37 ya mwaka huu, ya mlalamikaji kuiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo. 
Kesi hiyo sasa itatolewa maamuzi maalum kesho saa 4 asubuhi.
Katika kesi hiyo, mawakili wa serikali wanaongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali, Dk.Tulia Ackson huku upande wa mlalamikaji ukiongozwa na Peter Kibatala.
Shauri hilo lililofunguliwa na Mgombea Ubunge Viti Maalumu Jimbo la Kilombero (Chadema), Amy Kibatala, akitaka mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.