Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
HABARI mjini kwa sasa ni kuhusu tetesi
za kuachana kwa ‘flawaz’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mzazi
mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Kuna madai kwamba
biashara yao imefika tamati baada ya mrembo huyo kutoka Uganda kumzalia
Diamond, mtoto aitwaye Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ na kutimkia
nchini Afrika Kusini (Sauz).
Huku
bado tetesi hizo hazijakauka masikioni mwa mashabiki, tayari
zilishaibuka nyingine kuwa staa huyo anayekimbiza Afrika huenda akamteka
Miss Dunia (2000) kutoka India, Priyanka Chopra na kumuweka kwenye
himaya yake hasa pale watakapokutana jijini Milan, Italia kwenye Tuzo za
MTV Europe Music (EMA).
Katika tuzo hizo, Diamond na Chopra wanachuana katika kipengele kimoja cha Msanii Bora (Best Worldwide Act: Africa/India).
Endapo ni kweli Diamond na Zari ndiyo
wamefika Kigoma, mwisho wa reli na amepanga kweli kufanya yake kwa
Chopra, swali ni je, atamuweza kulingana na thamani aliyonayo?
THAMANI YA CHOPRA
Chopra anatajwa kuwa msanii ghali zaidi
nchini India akiwa na utajiri unaofikia Dola za Marekani milioni 54
ambazo ni zaidi ya Sh. bilioni 100 kwa fedha za Kitanzania. Ukiachana na
utajiri huo, sifa na jina kubwa alilonalo duniani, mrembo huyo amewahi
kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na wasanii wenye majina makubwa
duniani.
Baadhi yao ni Aseem Merchant (muigizaji)
aliyekuwa mpenzi wake wa kwanza ambaye alimwagana naye baada ya
msichana huyo kushinda taji hilo la Urembo wa Dunia mwaka 2000. Baada ya
hapo, Chopra alinasa kwa mkali wa sinema za Bollywood nchini India,
Akshay Kumar kabla ya kuchukuliwa na Harman
Baweja waliyedumu kwa muda wa miaka
mitano kwenye uhusiano. Chopra alipomwagana na Baweja alizama kwenye
penzi la Shahrukh Khan (mfalme wa filamu India) kisha akahamia kwa
Shahid Kapoor ambapo inaelezwa kuwa ameachana naye hivi karibuni hivyo
yupo ‘singo’.
Ukweli ni kwamba, kuna kila sababu ya
Diamond kujipima ubavu kuwa kipato chake anachoingiza kwenye shoo moja
kisichopungua Sh. Milioni 10, umaarufu alionao na mali anazomiliki
kutosheleza kumshawishi mrembo huyo aliyewashinda vigogo kama Shahrukh
Khan wenye utajiri wa zaidi ya Sh. bilioni 200 za Kibongo.
Ikumbukwe kwamba, kwa wasanii wengi hasa
wa kimataifa, uhusiano wa kimapenzi ni moja ya vitu ambavyo vinatakiwa
kuwapa chati ili kuwasimamisha kibiashara, sasa ikiwa Diamond, 26,
hafurukuti kwa mrembo huyo kwa utajiri, umaarufu na umri, bado swali
litabaki palepale kuwa atamuweza?
HISTORIA INAMBEBA DIAMOND
Mbali na vigezo vyote hivyo kuonekana
kuwa juu ya uwezo wa Diamond kummiliki Chopra, bado historia inambeba
ikimuonesha katika suala zima la mapenzi kuwa ni mtu wa kujaribu na
kufanikiwa. Diamond aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mrembo wa
Tanzania (2006), Wema Sepetu wakiwa hawaendani hadhi.
Wema alionekana kuwa juu kwani tayari
alikuwa ana jina kubwa kitambo, jambo lililochangia kumpandisha chati
Diamond kwa kasi ya ajabu. Huo ni mfano mmojawapo tu unaoonesha kuwa kwa
Diamond lolote linaweza kutokea kiasi cha kuonesha maajabu ya kumnasa
mrembo huyo mwenye jina kubwa duniani, lakini katika hali halisi Diamond
ana kazi kubwa ya kujibu swali kwa kudhihirisha kuwa anamuweza mrembo
huyo pale atakapommiliki?

Note: Only a member of this blog may post a comment.