Musa mateja
Usipime! Ndugu, jamaa na marafiki wa staa bab’kubwa Afrika Mashariki
na Kati, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, wikiendi iliyopita wamekula
bata la hatari katika sherehe ya kuzaliwa kwa msanii huyo, Ijumaa
Wikienda linaripoti.
Burudani na raha hizo zilifanyika nyumbani kwa Diamond, Madale- Tegeta
jijini Dar, usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita na kuhudhuriwa na mastaa
kibao.
‘Diamond Platnumz’, akimwagiwa Soda na meneja wake.
MADEMU, VINYWAJI VYATAWALAHuku likiwa na mwaliko rasmi, gazeti hili liliwashuhudia mademu ‘classic’ wakijiachia mjengoni humo huku vinywaji laini na pombe kali vikichukua nafasi kubwa katika suala la burudani.
Mbali na hayo, baadhi ya waliofika kwenye hafla hiyo walijivinjari kwa kuogelea, kucheza muziki, kupiga mitungi na kadhalika hivyo kufanya shughuli hiyo kugubikwa na shangwe ya kufa mtu.
MAZINGIRA RAFIKI
Mazingira ya nyumbani kwa Diamond yaliwafanya karibu wageni wote waliofika kwa mara ya kwanza kujisikia burudani, kwani Diamond alionekana kujipanga na kupafanya nyumbani kwake kuwa ni mji wenye heshima ya kistaa tofauti na nyumba nyingi za mastaa wengine wa Bongo.
…Akikata Keki
FULL VINYWAJIEneo la kaunta iliyopo pembeni mwa bwawa la kuongelea lilikuwa limefurika kwa vinywaji kiasi kwamba hakuna mgeni aliyehitaji kinywaji na kukosa.
MASTAA WALIOIBUKA
Baadhi ya mastaa waliojitokeza katika sherehe hiyo ni pamoja na Salama Jabir, Rita Paulsen ‘Madam’ Ambwene Yessayah ‘AY’, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Hamis Mandi ‘B-Dozen’, Shadee Weris, Khaleed Mohamed ‘TID Mnyama’, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’, Babu Tale, Fella na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye alitinga mahali hapo usiku mnene na kujumuika na mastaa hao kwa burudani mbalimbali zilizokuwa zikiendelea.
Shilole nae alikuwepo.
BETHIDEI YENYE WADHAMINIAkizungumza na gazeti hili, mmoja wa mameneja wa Diamond, Salam alisema kwamba, maandalizi ya sherehe hiyo yalifanikishwa na uongozi wake huku wakipigwa tafu kubwa na wadhamini wao ambao ni Kampuni ya Cocacola na Serengeti.
Alisema kuwa makampuni hayo yaliwapatia vinywaji mbalimbali huku Diamond akitia mkono wake kufanikisha sherehe hiyo na kufanya gharama zote za kuandaa shughuli hiyo kuwa zaidi ya Sh. milioni 10.
DIAMOND ANENA
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye pati hiyo.
“Namshukuru Mungu kwa kuendelea kunilinda hadi kufikia tena siku hii
muhimu maishani mwangu, sina la zaidi ila nawashukuru tu wote
waliojitokeza kusherekea na mimi.“Kuna walioacha usingizi na familia zao, wengine wametoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar na kujumuika nami, hiyo ni ishara ya mapenzi ya dhati na upendo, nawashukuru wote waliofanikisha sherehe hii, bila wao nisingeweza kufanya kila jambo,” alisema Diamond.Makabrasha ya gazeti hili yanaonesha kuwa, Diamond sasa ametimiza umri wa miaka 26 tangu alipoliona jua Septemba 2, 1989.

Note: Only a member of this blog may post a comment.