Friday, October 16, 2015

Anonymous

Kuelekea Mechi Dhidi ya SIMBA Kesho, MBEYA City Imeendelea na Mazoezi Bila Kocha Mkuu! (+PICHAZ)

Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya ambayo  October 17 itaikaribisha Simba katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza mechi yake ya sita ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2015/2016. Mbeya City ambayo inashika nafasi ya 13 baada ya kucheza mechi sita na kushinda moja na kutoka sare moja inashuka uwanjani kucheza ikiwa na huzuni.

IMG-20151016-WA0018

Mbeya City kwa siku za hivi karibuni imeondokewa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Juma Mwambusi ambaye ameenda kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Yanga na kurithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa aliyepata mkataba wa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.

IMG-20151016-WA0014

Kwa sasa Mbeya City ina mkosa kocha wake mkuu na nahodha wa klabu hiyo Juma Nyosso ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa kwa kipindi cha miaka miwili, lakini kwa sasa wanafundishwa na kocha wao msaidizi Meja Abdul Mingange bila kuwa na kocha mkuu. Hata hivyo Mbeya City imeendelea na mazoezi ya kuelekea mchezo huo ikiwa na nyota wake kama Juma Kaseja na Haruna Moshi Boban.
IMG-20151016-WA0022

IMG-20151016-WA0020

IMG-20151016-WA0021
IMG-20151016-WA0019

IMG-20151016-WA0015

IMG-20151016-WA0016

IMG-20151016-WA0017

Boban na Kaseja

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.