Tuesday, October 20, 2015

Anonymous

Kilichomkuta Miss Tanzania Huyu Asiye na Skendo Ndoa Yake ya Ughaibuni...Avunja Ukimya na Kuanika Kila Kitu!

Miss Tanzania 2007, Richa Adhia.
Stori: Imelda Mtema
VUNJA ukimya! Miss Tanzania 2007, Richa Adhia ambaye amevunja rekodi kwa kutokuwa na skendo tangu anyakue taji hilo, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na ndoa yake ambayo alikuwa akitarajia kuifunga ughaibuni na mchumba wake wa muda mrefu, Hridhaan Dhllon. 
Akizungumza na gazeti hili, Richa alisema kuwa kila kitu kilienda sawa lakini kukawa na kikwazo kimoja kikubwa cha yeye baada ya kufunga ndoa kwenda kuishi nje na mumewe, jambo ambalo lilikuwa gumu kwake. “Taratibu zote zilikamilika lakini tulishindwana sehemu ya kuishi.Yeye alitaka tukaishi nje lakini ilishindikana hivyo na ndoa ikayeyuka, tumebaki marafiki tu wa kawaida,” alisema Richa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.