Na Imelda Mtema
Muigizaji wa muda mrefu, Sabrina
Rupia ‘Cath wa Mambo Hayo’, amekiri kuumia vibaya kufuatia kifo cha
aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe kutokana na ukaribu wao na
jinsi alivyokuwa na moyo wa kuwajali wengine.
Akizungumza kwa uchungu na mwandishi
wetu kwa njia ya simu kutoka Ludewa alikohudhuria mazishi ya mbunge
huyo, Cath alisema maumivu aliyonayo kamwe hayasimuliki na kwamba
itamchukua muda mrefu kumsahau Deo na kwamba ataendelea kumuombea kwa
Mungu, ampumzishe kwa amani.
“Nina maumivu makali, moyo wangu
umegubikwa na simanzi isiyo na kifani, kama unavyojua, Deo alikuwa
mpambanaji wa kweli, hakusita kutetea maslahi ya wananchi wa Ludewa na
taifa kwa ujumla, itanichukua muda mrefu kumsahau, familia zetu ni za
karibu mno,” alisema Cath.

Note: Only a member of this blog may post a comment.