Saturday, October 24, 2015

Anonymous

Hakuna Usafiri wa Mabasi October 25, Madereva Wameongea…(Audio)

Chama cha wamiliki wa mabasi nchini (TABOA) kimeamua kusitisha huduma zake zote siku ya October 25, ili kuwaruhusu madereva wake kupata nafasi ya kupiga kura katiaka kuchagua viongozi watao wafaa. 

Akizungumza na wanahabari mapema hii leo, muweka azima wa chama hicho bw. Issa Nkya amesema kwamba wanatambua kuwa wafanyakazi wao nao wanatakiwa kuungana na wananchi wengine katika kupiga kura.
“Sisi kama TABOA tumejipanga kuwapa ruksa wafanya kazi wetu ili kila mtu akapige kura kwakuwa ni jambo la msingi kwa kumchagua mtu atayemtaka.:- Issa 

Naye mwenyekiti wa chama cha wasafirishaji mkoani Kilimanjaro na Arusha Bw. Mohamed Alfa amewataka madereva kuhakikisha kuwa wanaongeza umakini katika kupiga kura ili kuepusha uwezekano wa kutokea kwa vurugu.
“kwanza kabisa tunawahasa mafanyakazi wetu tunawahasa kuepukana na ushabiki, dereva awe ni mtulivu na kuwa sehemu ya kuleta amani na ikitokea mabishano awaelimishe kwamba kila mtu kuwa na chama siyo uadui”
Bonyeza play kusikiliza mahojiano haya

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.