Staa wa Filamu za Kibongo, Ester Kiama juzikati alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvamiwa na vibaka na kuchezea kichapo kisha kuibiwa pesa na simu mbili.
Sosi
aliye karibu na staa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alidai kuwa,
siku ya tukio Ester alitoka viwanja na wenzake, walipofika Kijitonyama
jijini Dar yeye akiwa anaendesha gari, aliwashusha wenzake lakini wakati
anarudi kwenye gari ili aondoke, wakatokea vijana wawili na pikipiki
wakamfanyizia.
Ijumaa lilipopata taarifa hizo lilitinga nyumbani kwa Ester na
kumkuta akiwa hoi sambamba na majeraha, alipotakiwa kueleza kilichompata
alikiri kufanyiwa unyama huo ambapo alisema anajuta kutembea usiku bila
kuwa na mwanaume.

Note: Only a member of this blog may post a comment.