Imelda Mtema
MAKUBWA! Mzazi mwenziye
na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moses Iyobo, Mwengi amemtuhumu
mwigizaji Aunt Ezekiel kuwa ni mshirikina akidai amemrogea mwanaye.
Mwengi alisema hivi karibuni alimpeleka
mwanaye nyumbani kwa Aunt ili akamuone baba yake (Iyobo), lakini
alipomrudisha alikuwa katika hali mbaya.
“Mtoto karudi anaumwa, tumeenda
hospitali hatukuona tatizo hadi kwa wataalam wa jadi ndiko tulikopata
suluhu, ni Aunt tu atakuwa kamfanyia figisufigisu,” alisema Mwengi.
Baada ya Mwengi kumwaga madai hayo kwa Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu alimpigia simu Aunt ambapo alipopatikana, alimpuuza mwanamke huyo kwa kujibu kwa kifupi.
“Huyo anatafuta kiki kupitia jina langu, nimroge yeye kwa lipi? Si bora niwaroge watu wazima kuliko yeye mwendawazimu.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.