MGOMBEA urais
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli amemmwagia sifa lukuki,
mkali wao ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
kutokana na ushindi wa tuzo tatu za Afrimma zilizofanyika wikiendi
iliyopita nchini Marekani
“Ukweli
nampongeza sana msanii Diamond kwa jinsi anavyojituma na kuipeperusha
vyema bendera ya taifa letu…,” alisema Magufuli huku pia akiwapongeza
Ommy Dimpoz na Vanesa Mdee walioshinda tuzo tofauti katika
kinyang’anyiro hicho.
Aidha, katika kampeni hizo Magufuli
aliwaahidi wakazi wa mji huo kuwajengea Lindi mpya ambayo itakuwa ya
neema kupitia gesi inayopatikana kwenye ukanda huo, unafuu wa vifaa vya
ujenzi ikiwemo saruji ‘cement’ iliyoanza kupatikana kwa bei ya shilingi
8,000 kwenye kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara, zao la korosho ambalo
Magufuli alijinandi kuwa na digrii ya zao hilo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.