Klabu ya soka ya Arsenal ilikuwa ikihusishwa kutaka kuwasajili wachezaji kadhaa katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August lakini haikufanikiwa na hatimaye ilifanikiwa kumsajili kipa wa zamani wa Chelsea Peter Cech kwa dau la pound milioni 10, miongoni mwa majina yaliyokuwa yakitajwa kutaka kusajiliwa na Arsenal ni Karim Benzema, Edinson Cavani na Robert Lewandowski.
Robert Lewandowski
September 24 stori kutoka mtandao wa express.co.uk umeandika chanzo cha Arsenal kuwakosa nyota hao, licha ya Robert Lewandowski kutopewa kipaumbele katika klabu yake ya FC Bayern Munich chini ya kocha Pep Guardiola, wakala wa mchezaji huyo Cezary Kucharski alithibitisha kuwa Lewandowski haipendi hali ya hewa ya Uingereza.
Karim Benzema
Edinson Cavani
Kwa upande wa Edinson Cavani licha ya picha ya yeye akiwa pamoja na kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuvuja wakiwa Ufaransa, alinukuliwa kukiri kuhitajika na Wenger katika baadhi ya magazeti ya Ufaransa lakini amekuwa akiuhusishwa kujiunga na vilabu kadhaa katika dirisha la usajili la mwezi August lakini PSG ni mahali sahihi kwake na bado wanamuamini.
Wenger

Note: Only a member of this blog may post a comment.