Thursday, September 17, 2015

Anonymous

WOLPER Awatoa Hofu Mashabiki, Asisitiza Kubaki Kuwa Jacqueline LOWASSA

Staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper ambaye amejipambanua siasa kuwa anaunga mkono madadiliko kupitia UKAWA na kushiriki katika harakati za kumpigia kampeni Mh Edward Lowassa ambaye ni mgombea urasi kupitia UKAWA kwa tiketi ya CHADEMA, amewatoa hofu mashabiki wao kuwa hakuna bifu miongoni mwao kwani siasa zikiisha wataendelea na maisha yao kama kawaida tofauti na baadhi ya mashabiki wanavyodhani hasa baada ya wasanii hao wa bongo movies walivyotafautiana kimitazamo ya kisiasa kwakipindi hiki hadi kufia  kutoleana lugha kali miongoni mwao.

"Msijali Mashabiki siasa zikiisha maisha yetu yanaenda kama kawaida Maana sisi zetu kamera siyo viti vyekundu ila hapa pipozii tuu paka kieleweke"–Wolper aliandika kwenye mtandao wa instagram.
Pia kwenye moja ya posti zake kwenye mtandao huo huo Wolper alisisitiza kubaki kuwa team mabadiliko
“...Ni bora kuwa kaisari kuliko kuwa yuda mimi nitabaki kuwa Jacq Lowassa”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.