Hamida Hassan
Wasanii
mbalimbali wa filamu waliomo kwenye Kampeni za CCM kupitia mpango wa
Mama Ongea na Mwanao akiwemo Wema Sepetu, juzikati walimliza mama wa
msanii marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’ pale walipokwenda
kutembelea kaburi lake.
Wasanii hao walichukua uamuzi huo
walipopita katika kijiji alichozaliwa msanii huyo cha Lusanga, wilayani
Muheza mkoani Tanga na kwenda kumsalimia mama wa marehemu lakini
ilidaiwa kuwa Wema alimliza mama huyo baada ya kuonekana akilia sana
bila kunyamaza.
“Tulipofika pale tulionana na mama
Sharo, tukapiga naye stori mbili tatu lakini tuliona tusiishie pale,
tupelekwe kwenye kaburi la mwanaye, hapo ndipo alipoanza kubadilika na
kuonesha hali ya majonzi kisha akaanza kulia!
“Hali ile ilitufanya wote tuliokuwa pale
kupatwa na huzuni na kwa kweli wengi tulishindwa kujizuia kulia, hata
tulipofika kaburini, simanzi iliongezeka lakini tukaomba dua na
kuondoka,” alisema Halima Yahaya ‘Davina’ aliyekuwa mmoja wa wasanii
waliokuwa kwenye msafara huo.
1 comments:
Write commentsJAMANI KUHAMA CHAMA KIMOJA KWENDA CHAMA KINGINE NI HAKI YA KILA MTU, kama umeuona ukweli ulipo ufuate, dhana haita tufaidisha lolote ktk haki. yangu ni hayo tu
ReplyNote: Only a member of this blog may post a comment.