Wednesday, September 9, 2015

Anonymous

USWAHILINI Kuna Vituko! KICHANGA CHA MIEZI NANE CHATELEKEZWA KWA MJUMBE JIJINI DAR!

USWAHILINI kweli kuna vituko. Mambo mengine ukisimuliwa unaweza kuona kama sinema au hadithi, lakini ukikutana nayo mwenyewe ndiyo utajua kweli aisifuye mvua basi imemnyea kama anavyotuhabarisha Mjumbe wa Shina No. 24, Kata ya Kibamba, Wilaya ya Kinondoni, Kresencia Sanga.

Mjumbe huyo alisema yapata wiki moja na ushee iliyopita, mwanamke mmoja asiyefahamika alifika nyumbani kwake kwa nje na kumtelekeza mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi nane na yeye mwenyewe kutokomea kusikojulikana.

Alisema ilikuwa mchana wa saa nane hivi, akiwa sebuleni kwake na wanafamilia wengine wakiangalia televisheni, mjukuu wake mmoja alipoingia ndani na kwenda kuchota maji, aliyodai kutumwa na mtu aliyehitaji kunywa. Akiwa hana hofu yoyote, anasema mtoto huyo alitoka nje lakini baada ya muda alirejea akiwa na maji yake mkononi.

“Nilipomuuliza mbona anarudi na maji, akanijibu kuwa mtu aliyemtuma kakuta ameshaondoka, nikadharau tukaendelea na kuangalia tv.“Baada ya muda alifika mwanangu wa kiume na kuniita, kisha akaniuliza mbona tunaangalia televisheni huku nje kuna mtoto analia? Tulipotoka nje nyuma ya nyumba, tukamuona mtoto wa kike akiwa katika hali mbaya ya kiafya.

“Kutokana na hali hiyo ilibidi nimuogeshe yule mtoto na kwenda naye katika Ofisi za Serikali za Mtaa, tukakuta zimeshafungwa ikabidi niende Kituo cha Polisi Mbezi kwa Yusuph nao waliniomba nikalale naye mpaka kesho kwa kuwa askari wa Dawati la Jinsia hawakuwepo. Siku ya pili tulifika pale kituoni asubuhi na kutoa maelezo ya tukio nzima, wakamchukua yule mtoto na kumpeleka Ustawi wa Jamii.

Je, wewe ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Mtendaji au Mjumbe? Kama una kesi yoyote ya kusisimua uliwahi kukutana nayo tafadhali wasiliana nasi ili tuitoe kwa Watanzania kwa lengo la kujifunza.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.