Monday, September 14, 2015

Anonymous

Ufisadi CCM na UKAWA, LOWASSA na KIKWETE, CCM Zanzibar +Waislam wa Tz Mecca? (Audio).

Magazeti ya Jumatatu 14 September 2015 yako mtaani tayari kama uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita ninazo hapa zile zote kubwa kwenye vichwa vya habari leo..
Lowassa asema Kikwete ameshindwa kutimiza yale alioahidi kwa muda wa miaka 10 ya uongozi wake, Tindu Lissu amtaka Rais Kikwete aseme RICHMOND ya nani, Mbunge wa  CHADEMA  Lushoto Mohamed Mtoi afariki dunia kwa ajali ya gari.
CCM wazindua kampeni kwa kishindo Zanzibar, John Magufuli asema Serikali yake itatoa kipao mbele kwa wakulima na wafugaji, Rais Kikwete asema CCM ushindi hauwezekani bila watu wa Zanzibar kujipanga. 
Lori lavamia msafara wa mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Magufuli, CCM haibadiliki hata waje malaika asema Zitto Kabwe, Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi amesema hakuna taarifa za vifo vya waislam wa Tanzania walioenda kuhiji ibada Mecca.
 
Hoja ya ufisadi yaigawa CCM na UKAWA, Zanzibar imeanza mazungumzo na kampuni ya Shell Uingereza kwa ajili ya kuchimba mafuta, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imekemea vurugu, uvunjishi wa amani na fujo wakati huu wa kampeni, Rais Kikwete kuzindua barabara ya Maragarasi na Idadi ya mauzo Soko la Hisa Tanzania la shuka.
Nimerekodi uchambuzi wote wa magazeti kupitia #PowerBreakfast na kukuwekea hapa chini, bonyeza play kusikiliza.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.