MWANAMUZIKI wa Marekani, Rihanna, usiku wa jana, alikuwa kivutio kwa
midomo yake ambayo alikuwa ameipaka rangi za kuvutia katika maonyesho ya
fasheni yaliyofanyika jijini New York (NYFW).
Maonyesho hayo yalifanyika katika Hoteli ya Edition ambapo midomo
yake ilikolezwa vyema kwa rangi ya bluu akiwa amevaa gauni la kuvutia
jeupe ambalo ni bidhaa ya kampuni ya Ellery ya Australia.

Note: Only a member of this blog may post a comment.