Tuesday, September 8, 2015

Anonymous

Shoga Acha Ushamba, KIMINI Mvalie Mumeo Apagawe!

mini
Shoga, ni matumaini yangu kwamba hali yako ni nzuri na unaendelea na majukumu ya malezi ya familia pamoja na pilika za kutafuta mkate wa kila siku.
Kwa upande wangu sijambo nipo ofisini nawaandalia mada nyingine ya wiki ijayo, si unaelewa hapa ni kazi tu!
Leo shoga yangu nimeamua kuzungumzia uvaaji unaongeza mashamsham kwa wandani wetu hususan waume zetu lengo likiwa ni kuziboresha ndoa zenu.

Nimeamua kuzungumzia mada hii baada ya kubaini baadhi ya wenzetu walio kwenye ndoa huvaa nguo za nusu utupu na kukatiza mitaani bila soni.
Hivi mwanamke uliyeolewa inakuwaje kuvaa kimini cha kukata na shoka, pensi au suruali ya kubana kisha kukatiza mbele za watu?

Hivi ikitokea wanaume wakware wanakupigia miluzi au kukutongoza utasema hawana adabu? Hiyo siyo sawa kabisa.
Utamkuta mwanamke aliye kwenye ndoa au mchumba wa mtu kavaa nguo fupi na kushindwa kukaa kwenye siti ya daladala kwa sababu hipsi zote zinakuwa wazi na kuishia kujiziba kwa kutumia viganja au pochi.

Hivi kama bado unapenda mambo ya usichana kwa nini ulikubali kuolewa? Mbona unamuaibisha mumeo na wanao kama tayari una watoto?
Kwa ninavyoelewa mwanamke kuwa na nguo za mitigo kama vimini, pensi na suruali za kubana ni sawa lakini anapaswa kumvalia mumewe wakiwa chumbani au peke yao nyumbani.

Kumvalia mavazi hayo kutamfanya ahamasike kuwa na wewe eneo la kujidai kwa sababu ataona jinsi hipsi zako zilivyonona ikiwa na jinsi ulivyofungashia eneo la nyuma ambalo ni ugonjwa wa wanaume wengi .
Hapo nguo hizo za nusu utupu ndipo mahali pake lakini kuzivaa mitaani unajishushia heshima yako na ya mumeo. Bye!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.