Monday, September 14, 2015

Anonymous

Rais JK Ateua Wakuu wa Mikoa Wapya...AMOS MAKALA Aliyechemka Ubunge Ndani!

Amefanya uteuzi huo leo hii. Amos Makala anakuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na Jordan Rugimbana kuwa mkuu wa mkoa wa Lindi.

Mwantum Mahiza wa Lindi amehamishiwa kuwa RC Tanga kuchukua nafasi ya Said Magalula aliehamishiwa Rukwa.

Wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro na Rukwa ambao ni Stela manyanya na Leonidas Gama wameacha kazi kwakuwa wanagombea ubunge.

Wakuu hao wapya wanaapishwa kesho kutwa
UPDATE
Dr. Tulia Atson ameteuliwa kuwa Naibu mwanasheria mkuu wa serikali kuanzia sasa. Dr Tulia anakumbukwa sana kwa michango yake katika Bunge la Katiba

UPDATE 2
BI Mary Longway Jaji mstaafu na Bi Asina Omary wameteuliwa kuwa makamishna wapya wa Tume ya taifa ya uchaguzi. Teuzi zinaendelea kutangazwa na Ikulu na naendelea kuwawekea hapa

UPDATE 3
Rais amemteua Profesa Mohamed Bakari Kambi kutoka Chuo kikuu cha afya Muhimbili kuwa Mganga mkuu wa serikali

UPDATE 4
Rais amemteua Bw Mlingi Elisha Mkucha kuwa mtendaji mkuu wa shirika la Maendeleo Tanzania NDC.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.