BRIGHTON MASALU
MSANII wa muziki wa Injili, Sarah Mvungi amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa ana gundu na wanaume na kwamba wengi humkimbia kutokana na sharti analowapa.
Akizungumza na Amani, Sarah alisema katika maisha yake hajawahi kufurahia mapenzi, aliwahi kuishi kwenye ndoa kwa miaka 12 lakini hakuwahi kufurahia maisha ya kuolewa.
“Si kwamba sitongozwi, la hasha, natongozwa tena wengi wanakuja kwa
gia ya kutaka kunioa lakini kila mwanaume anataka kushiriki tendo la
ndoa kwanza kabla ya ndoa, jambo ambalo sipo tayari kuliruhusu kwa kuwa
mimi ni mtumishi wa Mungu mwenye hofu ya dhambi.
“Mwanaume nikimpa sharti hilo, anakimbia na harudi tena, yaani ni kama nina gundu lakini naamini Mungu atanipa mwanaume wa kuendana na mimi,” alisema Sarah.
MSANII wa muziki wa Injili, Sarah Mvungi amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa ana gundu na wanaume na kwamba wengi humkimbia kutokana na sharti analowapa.
Akizungumza na Amani, Sarah alisema katika maisha yake hajawahi kufurahia mapenzi, aliwahi kuishi kwenye ndoa kwa miaka 12 lakini hakuwahi kufurahia maisha ya kuolewa.
“Mwanaume nikimpa sharti hilo, anakimbia na harudi tena, yaani ni kama nina gundu lakini naamini Mungu atanipa mwanaume wa kuendana na mimi,” alisema Sarah.

Note: Only a member of this blog may post a comment.