Wednesday, September 2, 2015

Anonymous

MUNGU ATUEPUSHIE MACHAFUKO UCHAGUZI -TIKO

Gladness Mallya
STAA wa filamu Bongo, Tiko Hassan amemuomba Mungu aiepushe Tanzania na machafuko wakati huu taifa likijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani hapo Oktoba mwaka huu.

Staa wa filamu Bongo, Tiko Hassan.
Akipiga stori na gazeti hili, msanii huyo aliwataka watu kutofanya mambo kwa kufuata mkumbo kwani uchaguzi unaonekana kuwa mgumu wenye mchuano mkali baina ya vyama vyote vya siasa.
“Nina wasiwasi sana na uchaguzi wa mwaka huu, kwani lolote linaweza kutokea, hivyo Watanzania wanatakiwa kuwa makini na kuachana na tabia ya kufuata mkumbo kwani hali inavyoonekana tusipokuwa makini vurugu zinaweza kutokea hivyo tumuombe Mungu sana,” alisema Tiko.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.